SiasaKorea Kaskazini
Korea Kaskazini yaidhinisha mkataba wa ulinzi na Urusi
12 Novemba 2024Matangazo
Shirika la Habari la Korea Kaskazini (KCNA) limesema mkataba huo "uliidhinishwa kama amri" ya Kim Jong Un, likimtaja kama "Rais wa Masuala ya Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea."
Notisi hiyo inajiri baada ya wabunge wa Urusi kupiga kura kwa kauli moja wiki iliyopita kuuidhinisha mkataba huo, ambao Rais Vladimir Putin aliutia saini baadaye.
Rais Vladimir Putin na Kim walitia saini mkataba wa ushirikiano wa kimkakati mwezi Juni, wakati wa ziara ya Putin mjini Pyongyang, ukiyataka mataifa yote mawili kusaidiana mara moja kijeshi ikiwa mmoja wao atashamuliwa na kushirikiana kimataifa kupinga vikwazo vya Magharibi.
Mkataba huo utaanza kutekelezwa baada ya pande hizo mbili kubadilishana hati za uidhinishwaji, limesema KCNA.