Korea Kaskazini yajibu luteka za kijeshi za Marekani
11 Agosti 2021Matangazo
Afisa mwandamizi wa Korea Kaskazini Kim Yong Chol ameilaani Korea Kusini kwa kuendeleza luteka hizo za pamoja na kuonya kuchukua hatua zisizojulikana ambazo zitaifanya Seoul kutambua kuwa imejiingiza katika mgogoro wa usalama. Siku moja kabla, Kim Yong Jong, dadake mwenye nguvu wa kiongozi wa Korea Kaskazini, alisema mazoezi hayo ni ishara ya wazi ya sera ya uchokozi ya Marekani kuelekea Pyongyang. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani Ned Price amesisitiza kuwa Marekani kwa muda mrefu haina nia ya uhasama na Korea Kaskazini. Amesema nchi yake inaunga mkono mazungumzo ya Korea hizo mbili na itaendelea kushirikiana na Korea Kusini ili kufanyikisha hilo.