1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kaskazini yajibu tamko la NATO

13 Julai 2024

Korea Kaskazini imelaani tamko lililotolewa na NATO, lililolaani mauzo ya silaha za Pyongyang kwa Urusi, likisema si halali. Jumuiya hiyo iliilani Korea Kaskazini kwa kuchochea vita vya Urusi dhidi ya Ukraine

 Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: Korea News Service/AP/picture alliance

Korea Kaskazini imelaani tamko lililotolewa katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya kujihami, NATO, lililolaani mauzo ya silaha za Pyongyang kwa Urusi, likisema si halali. Katika tamko la pamoja lililotolewa Julai 10 mjini Washington viongozi wa NATO waliilani Korea Kaskazini kwa kuchochea vita vya uchokozi vya Urusi dhidi ya Ukraine kwa kutoa msaada wa moja kwa moja wa kijeshi kwa Urusi.

Soma zaidi. Korea Kaskazini yakosoa tamko la mkutano wa kilele wa NATO, linaloishutumu kwa kuisaidia Urusi

Shirika la habari la Korea Kaskazini KNCA limeripoti leo kwamba wizara ya mambo nje inalaani kwa nguvu na kulikataa tamko la NATO. Likimnukuu msemaji wa wizara hiyo, shirika hilo limesema tamko hilo linachochea vita vipya baridi na makabiliano ya kijeshi katika ngazi ya kimataifa na nguvu na mbinu mpya zinahitajika kukabiliana na hali hiyo. 

Korea Kaskazini mara kwa mara imekuwa ikikanusha madai kwamba inasafirisha silaha kwenda Urusi, lakini mnamo mwezi Juni mwaka huu kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un na rais wa Urusi Vladimir Putin walisaini mkataba unaojumuisha ahadi ya kusaidiana kijeshi wakati nchi zao zitakaposhambuliwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW