SiasaKorea Kaskazini
Korea Kaskazini yajitayarisha kinyuklia kuidhibiti Marekani
3 Februari 2023Matangazo
Tamko hilo hilo la Korea Kaskazini kupitia wizara yake ya mambo ya kigeni limetolewa kujibu matamshi ya waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin aliyesema mapema wiki hii kwamba Washington itaongeza kiwango cha silaha za kisasa kwenye rasi ya Korea.
Austin aliyekuwa ziarani nchini Korea Kusini aliahidi kupelekwa kwa ndege zaidi za kivita pamoja na manuari za Marekani na kumarisha mazoezi ya kijeshi kati yake na Korea Kusini.
Korea Kaskazini iliyo hasimu wa Korea Kusini imesema kutanuka huko kwa shughuli za kijeshi kwenye rasi ya Korea kunalifanya eneo hilo kuwa uwanja hatari wa kivita na Pyongyang itajibu kwa kuimarisha uwezo wa kijeshi hususani silaha za nuyklia.