1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kaskazini yakanusha kupeleka wanajeshi Urusi

22 Oktoba 2024

Korea Kaskazini imekanusha kupeleka wanajeshi wake Urusi kuisaidia Moscow katika vita vyake dhidi ya Ukraine na kuyaita madai hayo kuwa yasiyo na msingi.

Korea Kaskazini Pyongyang | Kim Jong Un na Vladimir Putin
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, katikati kulia, na Rais wa Urusi Vladimir Putin, katikati kushoto, wakiondoka baada ya kufanya mkutano katika nyumba ya wageni ya serikali huko Pyongyang, Korea Kaskazini, Jumatano, Juni 19.Picha: Korean Central News Agency/Korea News Service/AP/picture alliance

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Korea Kaskazini wakati wa Mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa. Mwakilishi huyo amesema ujumbe wake hauoni haja ya kutolea ufafanuzi kuhusu ushirikiano wa kijeshi kati ya Pyongyang na Urusi. Kauli hiyo imetolewa ikiwa ni majibu ya shutuma zilizotolewa Ijumaa na Shirika la Ujasusi la Korea Kusini kuwa Pyongyang ilipeleka wanajeshi takriban 1500 Urusi na tayari wanapatiwa mafunzo kabla ya kuelekea katika uwanja wa mapambano. Pyongyang na Moscow zimekuwa washirika tangu kuanzishwa kwa Korea Kaskazini baada ya vita vya pili vya dunia. Nchi hizo zimekuwa karibu zaidi tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mwaka 2022. Tangu wakati huo Marekani imekuwa ikimtuhumu kiongozi wa Pyongyang Kim Jong Un kwa kupeleka silaha Urusi ili zitumike dhidi ya Ukraine.