SiasaAsia
Korea Kaskazini yakataa kuendelea na mazungumzo na Kusini
28 Julai 2025
Matangazo
Dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Yo Jong, amesema kwenye taarifa yake kupitia shirika la utangazaji la nchi yake kwamba Korea Kaskazini haina haja ya kuingia kwenye majadiliano na Kusini,licha ya wito wa rais mpya, Lee Jae Myung, ambaye anajaribu kuachana na siasa za uhasama za mtangulizi wake.
Kwenye ripoti iliyotangazwa leo, Kim Yo Jong, ambaye anaaminika kuwa na ushawishi mkubwa kwenye utawala wa kaka yake, Kim Jong Un, amesema Korea Kusini isitegemee kamwe kwa Kaskazini kuvutika na ahadi zake za uongo kuhusu mapatano.
Kim Yo Jong amedai kuwa mahusiano baina ya pande hizo mbili yameshaharibika mno kiasi cha kwamba hayarekebishiki tena.