1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini yarusha kombora baharini

8 Aprili 2026

Korea Kaskazini imerusha kombora kwenye bahari karibu na ufukwe wake katika pwani ya mashariki ikiwa ni tukio la pili ndani ya siku mbili, Hayo yamesemwa na jeshi nchini Korea Kusini.

2026 I Korea kaskazini
Kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: Yonhap/picture alliance

Korea Kaskazini imerusha kombora kwenye bahari karibu na ufukwe wake katika pwani ya mashariki ikiwa ni tukio la pili ndani ya siku mbili, Hayo yamesemwa na jeshi nchini Korea Kusini.

Tukio hilo limetokea baada ya jeshi la Korea Kusini kusema kuwa limegundua uzinduzi wa kombora lisilojulikana karibu na mji mkuu wa Korea Kaskazini siku ya Jumanne na kwamba mamlaka ya ujasusi ya Korea Kusini na Marekani zinaendelea kufanya uchunguzi kubaini kinachoendelea.

Mapema wiki hii, Korea Kaskazini ilisema kwamba kiongozi wake, Kim Jong Un alishuhudia jaribio la injini ya mafuta iliyoboreshwa kwa ajili ya silaha na kupongeza hatua hiyo aliyoitaja kuwa inaimarisha silaha zake za kimkakati kwa ajili ya shughuli za kijeshi nchini humo.

Hata hivyo,  katika tukio hili la hivi karibuni, timu ya maafisa wa Korea Kusini hawakutoa maelezo zaidi kuhusu umbali gani kombora hilo la Korea Kaskazini liliruka na aina ya kombora lenyewe.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW