Migogoro
Korea Kaskazini yarusha kombora wakati wa ziara ya Blinken
7 Januari 2025Matangazo
Kombora hilo lilielekezwa Bahari ya Mashariki (Bahari ya Japan) na kuanguka baharini, kwa mujibu wa taarifa za Japan. Huu ulikuwa uzinduzi wa kwanza wa Korea Kaskazini mwaka huu, baada ya majaribio ya kombora la kisasa la ICBM Novemba.
Uhusiano wa kijeshi kati ya Korea Kaskazini na Urusi umeimarika tangu uvamizi wa Moscow nchini Ukraine, na makubaliano ya kiulinzi yaliyotiwa saini Juni yameanza kutekelezwa.
Hali ya kisiasa Korea Kusini imezorota baada ya mzozo wa kisiasa, huku nchi hiyo ikiwazia kubadilisha sera yake ya kutotuma silaha za kivita kwa Ukraine.