1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini yarusha makombora kadhaa baharini

28 Januari 2024

Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa Korea Kaskazini ilirusha makombora kadhaa katika Pwani yake ya Mashariki.

Korea Kaskazini yafanya majaribio ya kombora
Watu wanatazama televisheni inayoonyesha matangazo ya habari yenye kanda ya jaribio la kombora la Korea Kaskazini.Picha: JUNG YEON-JE/AFP

Hii ikiwa ni mara ya pili kwa Pyongyang kufanya majaribio ya aina hiyo ya silaha katika kipindi chini ya wiki moja.

Kulingana na taarifa hiyo makombora hayo yalirushwa majira ya saa mbili asubuhi na kwamba mamlaka za kiitelijensia za Marekani na Korea Kusini zinafanya tathmini.

Hata hivyo haikuelezwa ni makombora mangapi yaliyorushwa na kiasi cha umbali yaliyosafiri.

Soma pia: Korea Kaskazini yafanya luteka za kijeshi mpakani na Korea Kusini

Kauli ya jeshi imesema kuwa wakati Korea ya Kusini ikiendelea kuimarisha ufuatiliaji na umakini, nchi hiyo inaendelea kushirikiana kwa karibu kijeshi na   Marekani. Taarifa hiyo imeendelea kubainisha kuwa Seoul inaendelea kufuatilia ishara za zozote za ziada na shughuli za Korea ya Kaskazini.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW