1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kaskazini yasema iko tayari kukabiliana na uvamizi

29 Agosti 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amelitaka jeshi lake kuwa tayari kuingia kwenye mapigano ili kuzuia njama za wapinzani wake ambao amesema huenda wakaivamia nchi yake.

Kim Jong Un amedai utulivu katika rasi ya Korea unahatarishwa kutumbukia kwenye vita vya nyuklia.
Kim Jong Un amedai utulivu katika rasi ya Korea unahatarishwa kutumbukia kwenye vita vya nyuklia.Picha: KCNA/AP Photo/picture alliance

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali vya nchini Korea Kaskazini tamko la kiongozi huyo amelitoa wakati ambapo Marekani, Korea Kusini na Japan zilifanya mazoezi ya kijeshi ya majini ya pande tatu.

Luteka hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kukabiliana na vitisho vya mashambulizi ya nyuklia kutoka Korea Kaskazini.

Kim Jong Un katika hotuba yake ya kuadhimisha Siku ya Wanamaji nchini Korea Kaskazini siku ya Jumatatu alisema utulivu katika rasi ya Korea unahatarishwa kutumbukia kwenye vita vya nyuklia.

Ametoa mfano wa mkutano wa hivi karibuni kati ya Marekani, Korea Kusini na Japan ambapo makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa kiulinzi yalifikiwa ili kukabiliana na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.