1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini kusimama na Urusi hadi ipate ushindi Ukraine

1 Novemba 2024

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya nje wa Korea Kaskazini Choe Son Hui wakati hofu ikiongezeka kuwa nchi hiyo itaingia katika mgogoro wa Ukraine.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na rais wa Urusi Vladimir Putin
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Vladimir Smirnov/POOL/TASS/dpa/picture alliance

Korea Kaskazini imesema kuwa itasimama na Urusi hadi itakapopata ushindi katika vita vyake nhini Ukraine. Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya nje wa Korea Kaskazini Choe Son Hui wakati hofu ikiongezeka kuwa nchi hiyo itaingia katika mgogoro wa Ukraine. 

Soma: Marekani yasema Korea Kaskazini umetuma wanajeshi 10,000 Urusi

Hui ametoa kauli hiyo leo baada ya mazungumzo na waziri mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov mjini Moscow. Nchi za Magharibi zinasema maelfu ya wanajeshi wa Korea Kaskazini wako nchini Urusi na kuna uwezekano watatumika nchini Ukraine.

Lavrov ameusifu uhusiano wa karibu kati ya majeshi ya Moscow na Pyongyang. Amesema Urusi inaishukuru Korea Kaskazini kwa kuchukua msimamo wa wazi kuhusu matukio yanayoendelea nchini Ukraine. Marekani inasema askari 8,000 wanapewa mafunzo nchini Urusi na huenda wakapelekwa vitani nchini Ukraine.