1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yasema Korea Kusini ni kama taifa la "uadui"

17 Oktoba 2024

Korea Kaskazini imesema katiba yake sasa inaitambua Korea Kusini kama taifa la "uadui"

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: KCNA VIA KNS/AFP

Hii ni mara ya kwanza kwa Pyongyang kuthibitisha mabadiliko ya kisheria yaliyoagizwa na kiongozi wake Kim Jong Un mapema mwaka huu.

Kulingana na shirika la habari la taifa la Korea Kaskazini KCNA, hatua hiyo ni sehemu ya Korea Kaskazini kujitenga kikamilifu na Korea Kusini.

Wiki iliyopita, nchi hiyo ilifanya mkutano muhimu wa bunge ambapo wataalam walikuwa wanatarajia kwamba kutafanyika mabadiliko ya katiba.

Mahusiano kati ya Korea hizo mbili yalizorota tangu mwezi Januari ambapo Kim aliielezea Seoul kama "adui mkuu" wa nchi yake, na kudai kwamba kaskazini haina haja ya kujiunga tena na kusini.

China ambaye ni mshirika mkuu wa kidiplomasia na kiuchumi wa Korea Kaskazini inasema inafuatilia kwa karibu hali katika Rasi ya Korea.