1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
TeknolojiaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yashindwa tena kutuma satelaiti angani

24 Agosti 2023

Jaribio la pili la Korea Kaskazini kutuma satelaiti ya kijeshi angani limeshindwa baada ya roketi iliyobeba chombo hicho cha anga za juu kupata hitilafu ikiwa njiani.

Roketi ya Korea Kaskazini
Jaribio la Agosti, 24, 2023 lilikuwa la pili. Picha: KCNA/AP/picture alliance

Roketi hiyo ilishindwa kuendelea na safari kutokana na kile maafisa wa Taasisi ya Maendeleo ya Teknolojia ya Anga za Mbali ya Korea Kaskazini wamesema ni hitilafu kwenye mfumo wake wa dharura.

Taasisi hiyo imesema, safari ya roketi hiyo ilikwenda vizuri katika hatua mbili za awali na hitilafu ya kiufundi ilitokea wakati wa hatua ya tatu.

Korea Kaskazini ilikuwa inajaribu kwa mara nyingine kupeleka satelaiti angani baada ya jaribio kama hilo kushindwa hapo Mei 31.

Satelaiti hiyo iliyopewa jina la Malligyong-1 ingeisaidia Pyongyang katika operesheni zake za kijeshi.

Hata hivyo jaribio hilo limekoselewa na mataifa jirani ikiwemo Japan na Korea Kusini huku Marekani ikisema linakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa vinavyoizuia Korea Kaskazini kurusha vyombo vya masafa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW