Korea Kaskazini yataka kuimarisha uhusiano wake na Urusi
21 Januari 2024Hilo linafanyika katika wakati ambapo nchi hizo mbili zikishirikiana kujenga mshikamano wa kukabiliana na maadui zao kufuatia kuongezeka kwa mvutano na Marekani.
Akielezea mkutano wake wa wiki iliyopita na rais wa Urusi Vladimir Putin pamoja na waziri wake wa mambo ya nje Sergei Lavrov mjini Moscow, Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini Choe Son Hui amesema Putin alimhakikishia kuwa yuko tayari kufanya ziara Pyongyang.
Waziri wa Mambo ya nje wa Korea Kaskazini azuru Moscow
Korea Kaskazini imekuwa ikijaribu kuimarisha mahusiano yake na Urusi, baada ya kiongozi wake Kim Jong Un kuitembelea Urusi mwezi Septemba mwaka jana na kukutana na Putin.
Kim anajaribu kujiondoa katika mtego wa kutengwa kidiplomasia na kuimarisha nguvu zake wakati akiendelea kupingana na Washinton,Seol na Tokyo kufuatia madai ya silaha za nyuklia.