1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kaskazini yathibitisha kurusha kombora

7 Januari 2025

Korea Kaskazini imethibitisha kwamba imerusha kombora la masafa ya kati lenye uwezo wa kutembea kwa kasi na kufika mbali zaidi.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un.
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un.Picha: KCNA/AFP

Mamlaka inayohusika na makombora imesema kwenye taarifa iliyotolewa jana kwamba imefanikiwa kufanya majaribio ya aina mpya ya kombora hilo ambalo kasi yake inazidi kasi ya sauti.

Shirika la habari la Korea Kaskazini, KCNA, imesema kwenye taarifa yake ya leo kwamba kombora hilo lilifika umbali wa kilomita 1,500, na kwamba jaribio hayo yalisimamiwa na kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un.

Soma zaidi: Zelenskiy adai wanajeshi wa Korea Kaskazini wanauawa kwa wingi

Kim amenukuliwa na KCNA akisema wameamua kuunda kombora lenye uwezo huo kukabiliana na vitisho vya wale aliowaita "vikosi vya maadui wa dola."

Kurushwa kwa kombora hilo kunasadifiana na ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, kwenye eneo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW