Korea kaskazini yavurumisha makombora karibu na Korea Kusini
2 Novemba 2022kufuatia hatua hiyo ya Korea Kaskazini, Korea Kusini imetoa maonyo ya nadra ya uvamizi wa anga na kuvurumisha makombora yake kama hatua ya kujibu kile ilichokiita uchokozi huo.
Hii ni mara ya kwanza tangu Korea kaskazini kufanya majaribio yake ya makomborana moja kuangua karibu na ukanda wa maji wa korea Kusini, katika makombora mengi iliyovurumisha kwa siku moja.
Soma zaidi:Korea Kaskazini yarusha makombora mengine ya masafa ya mbali
Kombora hilo lilitua kwenye mstari wa mpaka wa majini na Korea Kaskazini ambao unabishaniwa kati ya mataifa hayo jirani kitendo kinatajwa na rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol kuwa ni kitendo cha uvamizi katika eneo hilo.
Afisa mmoja wa jeshi amesema silaha zilizotumiwa ni pamoja na AGM-84H/K ambayo wanauhakika imetengenezwa nchini Marekani ambayo hutumika kushambulia na inaweza kuruka hadi kilometa 270 na ikiwa na kichwa chenye uzito wa kilo 360.
Mamalaka ya Korea Kusini inasema makombora 14 yalivurumishwakutoka pwani ya mashariki na magharibi mwa Korea Kaskazini.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo mkurugenzi mkuu wa oparesheni katika jeshi la Korea Kusini Kang Shin Chul amesema waligundua makombora matatu ya masafa mafupi ya korea Kaskazini.
Amesema makombora hayo yaliondondoka katika pwani ya rasi ya mashariki na kuapa kwamba jeshi la nchi yake litajibu vikali kile alichokiita uchokozi wa jirani yake Korea Kaskazini .
"Ufyatuaji wa makombora wa leo kwa mara ya kwanza Kombora la Korea Kaskazini limetua karibu na eneo letu la pwani, kusini mwa mpaka wa bahari"
Aliongeza kwamba hatua hiyo kamwe haikubaliki na jeshi la nchi yake litajibu vikali dhidi ya kitendo hicho ilichokiita cha kichokozi.
Luteka za kijeshi za kujihami kati ya washirika
Ufyatuaji huu wa makombora unafanyika wakati ambapo Marekani na Korea Kusini ambao ni washirika wakifanya luteka za pamoja za angani wiki hii.
Hatua hii inaenda sanjari na Korea Kaskazini kutoa kitisho kisicho wazi kutumia silaha zake za nyukliahatua ambayo imezusha hofu kubwa miongoni mwa watu na jumuia za kimataifa.
Soma zaidi:Korea Kaskazini yafyatua kombora kuelekea Japan
kitisho hicho cha Korea Kaskazini ilizifanya Marekani na Korea Kusini kulipa gharama kubwa zaidi na mbaya katika historia- kuongezeka kwa matamshi yake makali yanayolenga mazoezi yanayoendelea kati ya wapinzani wake.
Hapo jana Jumanne msemaji wa Wizara ya Mambo yaNje ya Marekani alisema kwamba mazoezihayo yanayoendelea kati ya washirika hao wawili yalilenga kujihami na kuongeza kwamba Washington imeieleza wazi Korea Kaskazini kwamba haina chuki dhidi ya nchi hiyo.
Katika mazungumzo kwa njia ya simu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Korea Kusini Park Jin wametaja kuvurumishwa kwa makombora ya Korea kaskazini ni uchochezi wa kijeshi usio kifani na kulaani vikali hatua hiyo.