1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiKorea Kusini

Korea Kusini kutuma kisanduku cheusi cha Jeju Air Marekani

1 Januari 2025

Jopo la wapepelezi wa Korea Kusini wanaochunguza ajali ya ndege ya shirika la Jeju Air iliyosababisha vifo vya watu 179, wamesema watapeleka moja ya visanduku vyeusi vya ndege hiyo nchini Marekani kwa uchunguzi zaidi.

Ajali ya ndege | Muan | Korea Kusini
Wataalamu kutoka bodi ya kitaifa ya usalama wa usafiri wa Marekani (NTSB) na timu ya uchunguzi wa Marekani na Korea Kusini wanaangalia eneo la ajali ya ndege huko Muan, Korea Kusini, Jumanne, Desemba 31, 2024.Picha: Son Hyung-joo/Yonhap via AP/picture alliance

Wapepelezi wa Korea Kusini na Marekani, wakiwemo pia kutoka kampuni ya ndege ya Boeing, wamekuwa wakilichunguza eneo la Muan kulikotokea ajali hiyo tangu siku ya Jumapili.

Soma pia: Watu 179 wafariki katika ajali ya ndege Korea Kusini

Naibu Waziri anayehusika na masuala ya usafiri wa anga wa Korea Kusini Joo Jong-wan amesema visanduku vyote viwili vinavyorikodi mawasiliano ya ndege vimepatikana, ikiwemo kile kinachorikodi sauti katika chumba cha marubani.

Ndege hiyo ilikuwa imebeba watu 181 kutoka Thailand wakati ilipoanguka na kusababisha vifo vya abiria wote isipokuwa wahudumu wawili pekee wa ndege waliokolewa wakiwa hai.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW