SiasaKorea Kusini
Korea Kusini, Marekani kufanya luteka ya pamoja?
2 Januari 2023Matangazo
Luteka hizo huenda zikahusisha silaha za nyuklia za Marekani wakati kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akiitaja nchi hiyo jirani yake kama "adui asiye na shaka."
Kauli ya Yoon, katika mahojiano ya gazeti yaliyochapishwa leo, imetokea baada ya kutoa wito wa kujiandaa kwa vita.
Gazeti hilo la Chosun Ilbo limemnukuu Yoon akisema mipango na luteka za pamoja zinalenga utekelezaji bora wa Marekani juu ya kile alichokiita "uwezo wa Washington kuzuia mashambulizi dhidi ya washirika wake" na kwamba Marekani imekumbatia wazo hilo.
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, amesema "hawana lolote la kutangaza" alipouliza kuhusu kauli ya rais huyo wa Korea, na kuongeza kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umesalia imara.