1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKimataifa

Korea Kusini na Marekani kuanza luteka za kijeshi

12 Agosti 2024

Korea Kusini na Marekani zimetangaza kwamba luteka yao ya kila mwaka itaanza wiki inayokuja ikilenga kuimarisha uwezo wa pamoja wa kuzuia na kujilinda dhidi ya kitisho cha nyuklia kinachoongezeka kutoka Korea Kaskazini.

Manowari ya Marekani
Mazoezi hayo makubwa ya kijeshi yatahusisha utayari wa kujilinda na mashambulizi ya makomboraPicha: Lee Jin-man/AP/picture alliance

Maafisa wa jeshi wa pande hizo mbili wamearifu mazoezi hayo makubwa ya kijeshi kwa mwaka huu yatahusisha utayari wa kujilinda na mashambulizi ya makombora, hujuma za mtandao na teknolojia za mawasiliano pamoja na mbinu za uwanja wa uwanja wa vita.

Soma pia: Manowari ya Marekani yawasili Korea Kusini kwa luteka za kijeshi

Msemaji wa jeshi la Korea, Lee Sung Joon amesema kwa jumla askari 19,000 wa nchi hiyo watashiriki luteka hiyo. Upande wa Marekani haujaweka wazi idadi ya wanajeshi wake watakaoshiriki.

Kwa kawaida Korea Kaskazini huyazingatia mazoezi hayo ya kila mwaka kuwa kitendo cha kichokozi na mara kadhaa imejibu kwa kufanya kufyetua makombora yake ya masafa kuonesha ubavu na uwezo wake wa kijeshi.