1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kusini, Poland zalaani Kaskazini kupeleka askari Urusi

24 Oktoba 2024

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol na mwenzake wa Poland Andrzej Duda wamelaani hatua ya Korea Kaskazini ya kupeleka wanajeshi nchini Urusi kwaajili ya kushiriki kwenye vita dhidi ya Ukraine.

Picha za satelaiti zikidai kuonesha askari wa Korea Kaskazini nchini Urusi
Wabunge wa Korea Kusini walisema Korea Kaskazini imepeleka wanajeshi 3,000 UrusiPicha: Sopa/Sipa/picture alliance

Viongozi hao wamesema hatua hiyo ni kitisho kwa usalama wa dunia na kwamba ni ukiukaji wa moja kwa moja wa maazimio ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Soma pia: Seoul: Huenda wanajeshi wa Korea Kaskazini wanapigana Ukraine

Rais Yeol wa Korea Kusini amesema nchi yake itachukuwa hatua. "Nimeweka wazi kwamba Jamhuri ya Korea Kusini haitoruhusu hiki kifanyike na itachukua  hatua zinazostahiki pamoja na Jumuiya ya Kimataifa dhidi ya ushirikiano wa kijeshi kati ya Urusi na Korea Kaskazini.'' Amesema Yeol. 

Wabunge wa Korea Kusini walisema baada ya kupata taarifa kutoka shirika la ujasusi la nchi hiyo,kwamba Korea Kaskazini imepeleka wanajeshi 3,000 Urusi.  Marekani pia imesema ina ushahidi unaoonesha Korea Kaskazini imetuma idadi hiyo ya wanajeshi Urusi.