1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Korea Kusini tayari kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini

15 Agosti 2024

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol amependekeza kuwepo "kundi la ushirikiano la Korea" linalolenga kupunguza mivutano na Korea Kaskazini.

Rais wa Korea ya Kusini
Rais wa Korea ya KusiniPicha: Kim Min-Hee/AP Photo/picture alliance

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol leo, amependekeza kuwepo "kundi la ushirikiano la Korea" linalolenga kupunguza mivutano inayoongezeka na Korea Kaskazini na kutafuta njia za ushirikiano wa kiuchumi.

Yoon ameyasema haya katika hafla ya kuadhimisha ukombozi wa nchi hiyo kutoka kwenye utawala wa kikoloni wa Japan, alipotangaza pia "maono yake ya kuungana kwa Korea hizo mbili." Mahusiano baina ya Korea hizo mbili kwa miaka sasa yamekuwa si mazuri, huku Korea Kaskazini hivi karibuni ikitangaza kupeleka makombora 250 ya masafa marefu katika mpaka wake wa kusini.

Korea Kaskazini pia imekuwa ikituma maelfu ya maputo yaliyojaa taka kwa jirani yake huyo wa Kusini tangu mwezi Mei, jambo lililoisababishia Korea Kusini kuanzisha tena matangazo ya propaganda katika mpaka wake na Korea Kaskazini na kusimamisha mkataba wa mwaka 2018 uliokuwa unalenga kupunguza mivutano baina ya majeshi ya mataifa hayo mawili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW