1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Korea Kusini yafanya mkutano kutafuta mkataba wa plastiki

Josephat Charo
25 Novemba 2024

Mkutano unafanyika saa chache baada ya kukamilika mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa COP29 mjini Baku, Azerbaijan.

Uchafu wa plastiki katika ufuo wa bahari
Uchafu wa plastiki katika ufuo wa bahariPicha: erta Olenick/SuperStock/IMAGO

Wawakilishi na wapatanishi kutoka nchi 175 wanakutana leo mjini Busan nchini Korea Kusini katika jitihada ya mwisho kuandaa mkataba wa kushughulikia mgogoro wa uchafuzi wa plastiki duniani.

Hii ni mara ya tano mataifa ya dunia yanakutana kuandaa mkataba wenye mafungamano ya kisheria.

Mbali na wajumbe wa mataifa tofauti, wawakilishi kutoka sekta ya utengenezaji wa plastiki, wanasayansi na wanamazingira wanahudhuria mkutano wa Busan kuchangia mawazo kutafuta njia ya kulishughulikia tatizo linaloongezeka la uchafuzi unaotokana na platiki.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mazingira la Umoja wa Matiafa UNEP Inger Andersen amesema sayari ya dunia inanyongwa na plastiki, huku maziwa, mito, bahari na miili ya binadamu ikiathriwa na uchafuzi wa plastiki.

Andersen amesema tatizo hili linaweza kutafutiwa ufumbuzi na lazima suluhisho lipatikane katika mkutano wa Busan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW