1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiKorea Kusini

Korea Kusini yawahamisha Skauti kutoka kambi ya Jamboree

Sylvia Mwehozi
8 Agosti 2023

Korea Kusini imeanza kuwahamisha makumi ya maelfu ya vijana kutoka kambi kubwa ya Skauti duniani kwa sababu ya tahadhari ya kutokea kwa dhoruba ya kitropiki.

Korea Kusini
Maskauti wakijiandaa kuondoka katika kambi ya JamboreePicha: Anthony Wallace/AFP/Getty Images

Korea Kusini imeanza kuwahamisha makumi ya maelfu ya vijana kutoka kambi kubwa ya Skauti duniani kwa sababu ya tahadhari ya kutokea kwa dhoruba ya kitropiki.

Kambi ya kimataifa ya Skauti ya Jamboree kwenye pwani ya magharibi ya Korea Kusini awali ilipangwa kudumu hadi Agosti 12, lakini imefupishwa kutokana na hofu ya Kimbunga Khanun

Vyombo vya habari vya Korea Kusini vimeripoti kwamba zaidi ya mabasi 1,000 yanatumiwa kusafirisha zaidi ya vijana 36,000 katika mji mkuu Seoul na mikoa mingine ya nchi.

Vijana wakiondoka kambi ya skauti ya JamboreePicha: Anthony Wallace/AFP/Getty Images

Vijana hao watakaa ndani ya hoteli, mabweni ya wanafunzi na vituo vya mafunzo. Kulingana na kikosi cha Ujerumani, washiriki wake 2,200 watakaa mjini Seoul na maeneo jirani hadi watakaporejea nyumbani.

Shirika la habari la Yonhap limesema kuwa waziri mkuu wa Korea Kusini Han Duk alisema uhamishaji huo ulikuwa ni hatua za tahadhari.

Ofisi ya hali ya hewa ya Korea Kusini imesema kimbunga hicho kikali kwa sasa kinaelekea kaskazini kuelekea Rais ya Korea na kinaweza kutua siku ya Alhamisi. Ofisi hiyo imesema upepo mkali na mvua kubwa vinatarajiwa. Hali ya hewa tayari imefanya mambo kuwa magumu kwa vijana hao wa Skauti hao, kwani wamekabiliwa na joto kali tangu mkutano huo uanze Saemangeum Jumanne iliyopita.

Maelfu ya washiriki kutoka Uingereza, Marekani na Singapore walikuwa tayari wameondoka kwenye kambi. Zaidi ya maskauti 43,000 kutoka nchi 158 walikuwa wamejiandikisha kwa kambi hiyo ambayo hufanyika kila baada ya miaka minne.