SiasaKorea Kusini
Korea Kusini yapanga kuwafidia waganga wa kazi za laazima
6 Machi 2023Matangazo
Hata hivyo waathirika wameukosoa mpango huo kwa sababu haujayafikia mapendekezo yao ya kutaka kuombwa radhi kikamilifu na Japan na kulipwa fidia moja kwa moja na makampuni ya Kijapani yaliyohusika na vitendo hivyo.
Pendekezo hilo lilikaribishwa mjini Tokyo lakini lilikabiliwa na upinzani wa mara moja kutoka kwa baadhi ya waathirika na kutoka chama kikuu cha upinzani cha Korea Kusini, ambao waliishutumu serikali kwa kusalimu amri kwa Japan.
Uamuzi huo wa Seoul umetangazwa wakati Korea Kusini na Japan zinaimarisha ushirikiano wa kiusalama kufutia ongezeko la vitisho kutoka Korea Kaskazini yenye nguvu za Kinyuklia.