Korea ya kaskazini yasema inaimarisha silaha zake.
4 Januari 2008Matangazo
Pyongyang.
Baada ya kushindwa kutimiza muda wa mwisho uliowekwa na jumuiya ya kimataifa kuweka wazi mipango yake ya kinuklia, Korea ya kaskazini imesema leo kuwa taifa hilo la kikomunist linapanga kuimarisha silaha zake za kivita. Gazeti la serikali ya Korea ya kaskazini pia limeishutumu Marekani kwa kuboresha silaha zake za kinuklia na kupanga vita vya kinuklia. Serikali ya Korea ya kaskazini imependekeza kuachana na nia yake ya kujipatia silaha za kinuklia ili kuweza kupatiwa msaada wa nishati pamoja na maridhiano ya kisiasa, na hadi sasa imekuwa ikishirikiana na China , Russia, Marekani na Korea ya kusini.