Korti ya juu Marekani yakataa kumkinga mshauri wa Trump
19 Machi 2024Hii ni baada ya kukaidi wito wa kamati iliyochunguza shambulio la mwaka 2021 dhidi ya bunge. Navarro, ambaye alihudumu kama mashauri wa biahsara wakati wa utawala wa Trump, alipaswa kuripoti gerezani kutumikia kifungo cha miezi minne kulingana na wakili wake.
Jaji Mkuu John Roberts, anaeshughulikia baadhi ya masuala ya dharura yanayohusisha kesi kutoka Washington DC, alikataa ombi la Navarro kwa niaba ya mahakama kuu.
Soma pia:Mshauri wa zamani wa Trump Navarro aamriwa kuripoti gerezani
Kamati ya majaji ilimtia hatiani Navarro Septemba mwaka jana kwa kukaidi bunge baada ya kugoma kuitikia wito wa kamati iliyokuwa inaongozwa na Wademokratiki, ikichunguza shambulizi la Januari 6, ambapo wafuasi wa Trump walivamia bunge kujaribu kuzuwia uidhinishaji wa ushindi wa rais Joe Biden.