1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korti ya kijeshi Uganda yasikiliza tena kesi ya Besigye

7 Januari 2025

Mahakama ya kijeshi ya Uganda ilianza tena kesi ya Kizza Besigye, mwanasiasa mkongwe wa upinzani aliyechukuliwa kwa nguvu kutoka majini Nairobi mwaka uliyopita, huku vurugu zikitokea mahakamani hapo.

Uganda | Kizza Besigye | Mwanasiasa wa upinzani
Mwanasiasa mkongwe wa upinzani wa Uganda, Kizza Besigye, aonyesha ishara alipowasili katika Mahakama ya Kijeshi ya Makindye jijini Kampala, Novemba 20, 2024.Picha: BADRU KATUMBA/AFP

Besigye alitekwa nyara mwaka jana kutoka Kenya alipokuwa Nairobi kuhudhuria uzinduzi wa kitabu ulioandaliwa na mwanasiasa wa upinzani wa Kenya na wakili, Martha Karua, kulingana na mke wake na makundi ya haki za binadamu. Besigye, kanali mstaafu mwenye umri wa miaka 68, anakabiliwa na mashtaka ya kumiliki silaha kinyume cha sheria na makosa mengine katika mahakama ya kijeshi.

Besigye alifika mahakamani pamoja na mshatakiwa mwenzake, Obeid Lutale, akiwa ameandamana na wakili wake mkuu, Martha Karua, ambaye Uganda ilimpa leseni ya muda ya kufanya mazoezi ya sheria nchini humo.

Awali, Karua alikuwa amezuiwa kufanya kazi ya uwakili nchini Uganda mwezi Desemba, hali ambayo ilikosolewa vikali na makundi ya haki za binadamu.

Besigye afikishwa mahakama ya kijeshi

01:16

This browser does not support the video element.

Soma pia: Martha Karua Kumtetea Dkt Kizza Besigye katika mahakama ya kijeshi Uganda.

Hata hivyo, wakili Erias Lukwago alieleza kuwa maafisa wa kijeshi walijaribu kuwazuia mawakili wa Besigye kuingia mahakamani, hali iliyosababisha vurugu kati ya wafuasi wa upinzani, mawakili, na vikosi vya usalama kabla ya kukamatwa kwa Kiiza.

Besigye, ambaye zamani alikuwa daktari binafsi wa Rais Yoweri Museveni, amekuwa akilengwa mara kwa mara na mamlaka tangu walipotofautiana mwishoni mwa miaka ya 1990, na amejaribu bila mafanikio kumshinda Museveni katika chaguzi nne.

Kesi hiyo inafanyika wakati ambapo Uganda imeongeza ukandamizaji dhidi ya wapinzani wa kisiasa, huku Museveni akitangaza ratiba ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2026, akieleza kuwa usajili wa wapiga kura utaanza Jumanne.

Tendo la kumfunga wakili bila mashtaka rasmi limeelezwa na Lukwago kama "dhuluma ya haki," akilaani pia jinsi mahakama ya kijeshi inavyowatendea washiriki wa kesi hiyo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW