1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Korti ya Uholanzi yafuta marufuku ya silaha kwa Israel

13 Desemba 2024

Mahakama moja nchini Uholanzi imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa na muungano wa makundi yanayoiunga mkono Palestina, iliyotaka kuizuia serikali ya nchi hiyo kusafirisha silaha kwenda Israel.

Mahaka yafuta marufuku ya silaha kwa Israel
Mahaka yafuta marufuku ya silaha kwa IsraelPicha: State Service for Export Control of Ukraine

Mahakama mjini The Hague imetupilia mbali madai yote na kusema hakuna sababu zozote za kuweka marufuku kamili ya usafirishaji wa vifaa vya kijeshi huko Israel.

Mashirika yasiyo ya kiserikali yamedai kuwa mamlaka za Uholanzi zilikuwa zikipuuza kuzuia kile walichokiita "mauaji ya kimbari" ya Israel huko Gaza.

Hayo yakiarifiwa, Israel imeendeleza mashambulizi yake katika Ukanda wa Mashariki ya Kati.

Mnamo Ijumaa Marekani ilisema kuna dalili zinazoleta matumaini ya kupatikana makubaliano ya kusitisha mapigano kwenye mzozo huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW