1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Korti ya Venezuela yatoa waranti kukamatwa Edmundo Gonzalez

3 Septemba 2024

Mahakama ya Venezuela imetoa hati ya kuwezesha kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani Edmundo Gonzalez.

Venezuela Marica Corina Machado eröffnet den Präsidentschaftswahlkampf in San Cristobal
Umati wa watu wamebeba mabango na kuandamana wakati wa ziara ya kisiasa ya kiongozi Maria Corina Machado katika eneo la San Cristobal, Venezuela, Juni 27, 2024.Picha: Jorge Mantilla/NurPhoto/picture alliance

Hatua hiyo imechukuliwa wiki moja baada ya wiki kadhaa za maandamano ya kuipinga serikali ya Rais Nicolas Maduro.

Mamlaka imesema imetoa hati hiyo baada ya Gonzalez kushindwa kufika mahakamani mara tatu kujibu maswali kutoka kwa waendesha mashtaka.

Kiongozi huyo wa upinzani Edmundo González, mwenye umri wa miaka 75, hajajitokeza hadharani tangu uchaguzi ulipomalizika.

Soma pia: Marekani yaikamata ndege ya rais wa Venezuela Nicolas Maduro

Mwendedesha mashtaka aliyetangaza hatua hiyo ya kukamatwa kwake amemlaumu kiongozi huyo wa upinzani kwa uhalifu ikiwa pamoja na mashtaka ya kula njama, kughushi hati na kutaka kupora mamlaka.

Mwanasheria mkuu wa Venezuela amesema mahakama imeikubali hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani kutokana na madai ya kutenda uhalifu mkubwa.