1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Kosovo yaruhusu magari ya Serbia na bidhaa kuvuka mpaka tena

17 Juni 2023

Mamlaka nchini Kosovo zimeondoa marufuku ya mpakani ya magari na bidhaa kutoka Serbia iliyowekwa siku tatu zilizopita, kituo cha televisheni cha serikali ya Serbia

Kosovo I Grenzschließung Serbien
Picha: Visar Kryeziu/AP/picture alliance

Hata hivyo kulingana na ripoti hiyo, ukaguzi wa malori na magari kutoka Serbia utaimarishwa katika vituo vya ukaguzi vya mpaka wa Kosovo, na kuruhusiwa kupita.

Soma pia: Mvutano kati ya Kosovo na Serbia wazidi kufukuta

Serikali ya Pristina iliagiza hatua hiyo ya kuzuia uingizwaji wa bidhaa kupitia mpakani Jumatano iliyopita baada ya Serbia kuwakamata maafisa wa polisi watatu. Kulingana na Kosovo, maafisa hao walikuwa wametekwa nyara huku Belgrade ikidai kwamba walikuwa wameingia Serbia.

Kikosi cha kulinda amani kinachoongozwa na NATO, KFOR kimesema mjini Pristina jana kwamba baada ya uchunguzi juu ya tukio hilo, hakikuweza kuthibitisha iwapo lilitokea Serbia ama Kosovo.