Kovac: Mustakabali wa Schlotterbeck uamuliwe kwa haraka
6 Machi 2026
Kovac lakini amesema ana imani kuwa Mjerumani huyo atasalia hapo Signal Iduna Park.
Schlotterbeck ana mkataba na Dortmundhadi mwaka 2027 na bado hajasema iwapo anataka kuurefusha mkataba huo. Iwapo ataamua kuwa anataka kuondoka basi Dortmund watalazimika kumuuza katika dirisha la uhamisho la kipindi cha majira ya joto, jambo ambalo litaathiri mipango ya kikosi kizima.
Katika siku chache zijazo kumepangiwa kufanyika mazungumzo kuhusiana na mkataba wa beki huyo wa kati na Kovac ana imani kuwa Schlotterbeck hataondoka klabuni hapo.
Dortmund watakuwa wanacheza na FC Cologne siku ya Jumamosi katika mechi ambayo ni muhimu kwao baada ya kulazwa na Bayern Munich katika mechi ya Der Klassiker mwishoni mwa wiki iliyopita 3-2 mjini Dortmund.
Bayern kwa sasa wako pointi 11 kifua mbele na Dortmund wako katika nafasi nzuri ya kushiriki Ligi ya Vilabu Bingwa msimu ujao lakini Kovac amewataka wachezaji wao wajitume na kutoa ushindi kwenye mechi dhidi ya FC Cologne.