1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine imesema vikosi vyake vipo chini ya shinikizo kali

28 Februari 2023

Ukraine imesema kuwa vikosi vyake vipo chini ya shinikizo katika mji wa Bakhmut, ambao umeharibiwa vibaya katika jimbo la mashariki la Donetsk ambalo Urusi imekuwa ikijaribu kulikamata kwa miezi kadhaa.

Ukraine Tschassiw Jar | Zerstörte Gebäude
Picha: Jose Colon/AA/picture alliance

Kamanda wa vikosi vya ardhini Oleksandr Syrskyi amesema kwenye mitandao ya kijamii kuwa hali karibu na Bakhmut ni tete. Amesema licha ya kukumbwa na hasara kubwa, adui ametumia vikosi vilivyojiandaa zaidi vya mashambulizi kutoka kundi la mamluki la Wagner, vinavyojaribu kuvunja ngome za majeshi ya Ukraine na kuuzingira mji huo.

Kitovu hicho cha kiviwanda ambacho kilikuwa na idadi ya wakaazi 70,000 kabla ya vita, kimekuwa uwanja wa vita mashariki mwa Ukraine. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alionya jana usiku kuwa hali karibu na Bakhmut inaendelea kuwa ngumu.