Putin yuko tayari kwa makubaliano ya amani Ukraine
20 Julai 2025
Peskov amesisitiza kuwa safari ya kufikia usitishaji wa mapigano Ukraine inahitaji uvumilivu na siyo rahisi.
Insert Peskov "Rais Putin amerejea kusema mara kadhaa juu ya shauku yake ya kufikisha mwisho mzozo wa Ukraine kwa njia ya amani haraka iwezekanavyo. Huo ni mchakato mrefu na unahitaji juhudi mahsusi na siyo kitu rahisi. Na inaonekana Marekani polepole itakuja kulielewa hili."
Vikwazo vipya dhidi ya Urusi katika njia panda
Rais wa Marekani Donald Trump amerejelea mara kadhaa matamshi yake ya kutaka kuumaliza mzozo wa Ukraine haraka lakini amesema amevunjwa moyo na tabia isiyotabirika ya rais Putin.
Jumatatu ya wiki hii, Trump alitangaza nia ya kuchukua msimamo mzito dhidi ya Urusi, akiahidi msaada mkubwa zaidi wa kijeshi kwa Ukraine, ikiwemo kuipatia mifumo mambo leo ya ulinzi chapa Patriot. Vilevile aliipatia Urusi muda wa mwisho wa siku 50 kufikia makubaliano ya kusitisha vita au ikabiliwe na vikwazo.