1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kremlin yakaribisha wito wa mazungumzo na Ulaya

16 Januari 2026

Urusi imekaribisha wito wa baadhi ya nchi za Ulaya kutaka kurejesha mazungumzo na nchi hiyo kuhusu mzozo wa Ukraine.

Dmitri Peskov,
Msemaji wa Ikulu ya urusi Dmitry Peskov amesema wito wa viongozi hao wa nchi za Umoja wa Ulaya unaonyesha mwelekeo mpya wa Ulaya.Picha: Mikhail Tereshchenko/TASS/ZUMA/picture alliance

Hatua hii inajiri baada ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni kueleza kuwa Ulaya inapaswa kuanza tena mawasiliano na Moscow.

Meloni amesema wakati umefika kwa Ulaya kuzungumza na Urusi, akifuata msimamo wa Macron ambaye Disemba alisema mawasiliano na Rais Vladimir Putin yanaweza kuwa "ya manufaa.”

Kuhusu wito huo Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema "Kwa nchi za Ulaya kulitambua hili na kutoa wito huu ni hatua itakayoleta maendeleo chanya.  Jambo hili linahitajika kutokea mapema au hata baadaye. Lakini hadi wakati huo, Urusi itaendelea kufuatilia malengo yake."

Msemaji wa Ikulu ya urusi Dmitry Peskov amesema wito wa viongozi hao wa nchi za Umoja wa Ulaya unaonyesha mwelekeo mpya wa Ulaya, akiongeza kuwa uthabiti wa bara hilo unahitaji mazungumzo na Urusi.

Kauli hizi zinatolewa wakati Marekani ikiendelea kuongoza juhudi za kutafuta suluhu ya vita vinavyoendelea kwa karibu miaka minne sasa kati ya Urusi na Ukraine.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW