1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Kremlin: Hakuna chochote kipya kufuatia kitisho cha Trump

23 Januari 2025

Ikulu ya Urusi imesema haijaona chochote cha msingi kwenye kitisho kipya kilichotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani cha kuiwekea vikwazo vipya na ushuru ikiwa haitakubali kuvimaliza vita vyake nchini Ukraine.

Russland Wladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Russian President Press Office/dpa/picture alliance

Kremlin imesema haijaona chochote cha msingi kwenye kitisho kipya kilichotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani cha kuiwekea vikwazo vipya na ushuru ikiwa haitakubali kuvimaliza vita vyake nchini Ukraine.

Soma pia: Marais wa Urusi na Iran wasaini makubaliano ya ushirikiano

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema hata katika awamu ya kwanza, Trump mara zote aliiwekea vikwazo Urusi na kurudia tena kwamba Urusi iko tayari kwa mazungumzo yenye usawa na kuheshimiana na Marekani.

Trump alisema jana kwamba ikiwa hawatafikia makubaliano hivi karibuni hatakuwa na chaguo jingine zaidi ya kuiwekea Urusi ushuru wa juu kabisa na vikwazo katika kila kitu kinachouzwa na Urusi nchini mwake pamoja na mataifa mengine washirika wa Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW