1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kremlin yasema Ukraine inaficha hali ya vikosi vyake

5 Novemba 2025

Urusi imeishutumu Ukraine kwa kuficha taarifa kuhusu kuzingirwa kwa wanajeshi wake katika miji ya mashariki ya Pokrovsk na Myrnohrad.

Urusi |  Dmitry Peskov akiwa Moscow
Msemaji wa Kremlin, Dmitry PeskovPicha: Pavel Bednyakov/Pool/REUTERS

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov, leo ameyaambia mashirika ya habari ya Urusi

kwamba Ukraine imekataa pendekezo la Urusi la kuitaka  kuruhusu waandishi wa habari wa nchi za Magharibi kutembelea eneo hilo, licha ya hamu yao kubwa.

Peskov alihoji kuhusu kinachofichwa Kiev akielezea hali ya kukata tamaa kwa  wanajeshi wa Ukraine.

Mara kwa mara, jeshi la Ukraine limekanusha madai ya Urusi ya kuzingira eneo hilo.

Putin aishauri Ukraine 

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameutaka uongozi wa Ukraine kufanya maamuzi kwa maslahi ya wananchi na wanajeshi wake, akimaanisha kuzingirwa kwa Pokrovsk na Kupiansk katika mkoa wa Kharkiv.

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema vikosi vyake huko Pokrovsk vitaendelea kuviangamiza vikosi vya Ukraine vilivyozingirwa, huku vikizuia mashambulizi kutoka Kiev.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW