KUALA LUMPUR: Ahadi ya kushirikiana zaidi kiuchumi
25 Julai 2006Matangazo
Nchi za Asia ya kusini-mashariki katika mkutano wa kilele nchini Malaysia leo hii zimeapa kuharakisha mpango wa kuanzishwa uhusiano wa kiuchumi kati yao.Tangazo hilo limetolewa baada ya mazungumzo ya Shirika la Biashara Duniani-WTO,kuvunjika siku ya jumatatu,mjini Geneva, Uswissi.Kuvunjika kwa mkutano wa WTO umesababisha lawama katika jumuiya ya kimataifa.Mkuu wa biashara wa Umoja wa Ulaya,Peter Mandelson ameituhumu Marekani inayokataa kupunguza ruzuku zinazolipwa kwa wakulima wa Kimarekani na kuathiri biashara duniani.