KUALA LUMPUR: Makosa yaliofanywa Irak yasirejewe
14 Oktoba 2006Matangazo
Malaysia imetoa mwito kwa madola makuu kutofikiria kutumia nguvu dhidi ya Korea ya Kaskazini kufuatia madai ya nchi hiyo kuwa imefanya jaribio la kinuklia.Waziri wa mambo ya kigeni wa Malaysia,Syed Hamid Albar amenukuliwa akisema,makosa yaliyofanywa nchini Irak yasirejewe.Malaysia iliyopinga vikali uvamizi wa Irak ulioongozwa na Marekani,imetoa mwito kwa Umoja wa Mataifa kuendelea kutumia diplomasia kuhusu Korea ya Kaskazini na imesisitiza kuwa mgogoro wo wote wa kijeshi utahatarisha usalama wa kanda nzima.Syed Hamid vile vile ameitaka Korea ya Kaskazini irejee katika majadiliano ya pande sita kuhusu mradi wake wa kinuklia.