1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KUALA LUMPUR: Mataifa ya kiislamu yataka mapigano yakome

3 Agosti 2006

Mataifa ya kiislamu yametoa mwito hii leo mapigano kati ya Israel na Hezbollah yakomeshwe mara moja. Muungano wa mataifa ya kiislamu umeonya mjini Kuala Lumpur nchini Malaysia, kwamba hasira inayozidishwa na mashambulio ya Israel nchini Lebanon huenda ikazusha wimbi jipya la ugaidi.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Lebanon, Fawzi Salloukh, amesema,

´Tunaitisha usitishwaji wa k udumu wa mapigano na kuondoka kwa wanajeshi wa Israel kutoka eneo la amani. Na pia kuanzishwe tume ya mahakama ya kimatiafa itakayochunguza matendo ya uhalifu yaliyofanywa na Israel. Tunata pia raia wa Lebanon warudi katika nyumba zao na miji yao.´

Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, aliyehudhuria pia mkutano wa muungano wa nchi za kiislamu mjini Kuala Lumpur, amenukuliwa akisema kandoni mwa mkutano huo kwamba kuingamiza Israel kutaumaliza kabisa mgororo wa sasa baina ya Israel na Hezbollah.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW