1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KUALA LUMPUR:Shirika la Amnesty Inernationali laitaka Malysia kukoma kuwatesa wakimbizi

20 Juni 2005

Leo ikiwa ndio siku ya wakimbizi duniani,Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty Inernationational hii leo limeitaka serikali ya Malysia kukoma kuwatesa wahamiaji haramu na badala yake shirika hilo limeitaka kuwaachilia huru wakimbizi waliofungwa.

Katika taarifa ya pamoja ya shirika hilo na makundi ya kutetea haki za binadamu nchini Malysia katika kuadhimisha siku hii ya wakimbizi duniani,Shirika la Amnesty limeitaka serikali hiyo kutowarudisha wakimbizi waliotoroka nchini mwao kwa ajili ya kuomba hifadhi ya kisiasa nchini humo.

Mwezi Marchi serikali ya Malysia ilianzisha operesheni kali ya kuwarudisha mamia ya wakimbizi walio nchini humo wengi wao wakiwa ni kutoka Indonesia:

Wahanga kati ya milioni tisa na 25 duniani kote wameelezwa kuwa wakimbizi wanaotafuta ufadhili katika mataifa yayoendelea ya magharibi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW