1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Kuleba kuelekea China kusaka suluhu ya mzozo wa Ukraine

22 Julai 2024

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ukraine Dymytro Kuleba anatarajiwa kesho Jumanne kwenda Beijing kwa mazungumzo yatakayojikita kuhusu kumaliza vita na Urusi pamoja na uwezekano wa China kubeba jukumu la kuwa msuluhishi.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ukraine Dmytro Kuleba
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ukraine Dmytro KulebaPicha: FADEL SENNA/AFP via Getty Images

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Ukraine atafanya mazungumzo hayo katika mkutano na mwenzake wa China Wang Yi mjini Beijing. Wizara ya mambo ya kigeni ya Ukraine imearifu kwamba mkutano huo utafanyika kesho hadi Alhamisi.

Soma pia:China imesitisha mazungumzo ya kudhibiti silaha na Marekani

Taarifa ya wizara hiyo pia imefafanuwa kwamba mazungumzo baina ya wanadiplomasia hao yatatuwana katika mjadala kuhusu namna ya  kuzuia uchokozi wa Urusi dhidi ya Ukraine.