1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroChina

Kuleba ziarani Beijing kutafuta amani nchini Ukraine

24 Julai 2024

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ukraine Dymitro Kuleba ambaye yuko ziarani Beijing, amesema ni muhimu kwa Ukraine na China -- ambayo ni mshirika wa karibu wa Urusi -- kuzungumza moja kwa moja kuhusu kumaliza vita Ukraine.

Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba
Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Kuleba yuko Beijing kukutana na viongozi wa ChinaPicha: Gleb Garanich/REUTERS

China inajipambanua kama mshirika asiyegemea upande wowote katika vita hivyo na kusema haitoi usaidizi hatari kwa pande zote mbili, tofauti na Marekani na mataifa mengine ya Magharibi. Hata hivyo, kuongezeka kwa ushirikiano wake "usio na ukomo" na Urusi kumesababisha wanachama wa NATO kuiita China kuwa "mwezeshaji madhubuti" wa vita vya Moscow, ambavyo serikali ya Beijing haijawahi kulaani.

Kuleba amesema atafanya mazungumzo ya kina na muhimu na waziri mwenzake wa China Wang Yi juu ya kufikia kile alichokiita "amani ya haki." Ziara ya Kuleba nchini China itakayokamilika Ijumaa, ni ya kwanza kufanywa na afisa yeyote wa ngazi ya juu wa Ukraine tangu Urusi ilipoivamia Ukraine Februari 2022.

Soma pia:Ukraine kuomba idhini pana ya kushambulia ndani ya Urusi

Beijing ilisema mazungumzo yatalenga mahusiano ya pande mbili na masuala mengine yenye maslahi ya pamoja.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW