1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kumbukumbu ya miaka saba ya mauwaji ya raia wa Beni

John Kanyunyu15 Oktoba 2021

Wakaazi wa Beni,Kivu ya Kaskazini wamefanya kumbukumbu ya miaka saba ya kile wanachokiita "Mauaji ya Mapanga" yaliyofanywa na waasi wa Uganda wa ADF.

Symbolbild | DR Kongo | Anschlag der Alliierte Demokratische Kräfte Kongo
Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Wakizungumza na idhaa hii kwenye makaburi ya Masiani mjini Beni, ambako walikuwa wanasafisha makaburi ya wahanga wa mauwaji ya Beni, wakaazi hawa walisema kile kilichowapelekea kufanya kazi hiyo ya pamoja maarufu, Salongo.

Mauwaji hayo ya kwanza kutokea katika mji wa Beni Oktoba kumi na tano mwaka wa elfu mbili na kumi na nne yalifanyika katika Kata ya Ngadi, nje kidogo na mji huu, siku ambayo waumini walikuwa wanakesha kumuomba Mungu katika kanisa la Kipentekoste, CEP.

Mchungaji Kyotha Kinanga wa kanisa hilo katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini, siku hiyo alikuwa anasimamia mwenyewe sala. Hapa anatuambia anachokikumbuka, huku akitoa wito kwa serikali kulinda watu pamoja na mali zao.

Soma pia:Vijana mjini Beni washika Doria kufuatia ongezeko la uhalifu

Ujenzi wa eneo la kumbukumbu

Picha: Reuters/S. Mambo

Na ili kuwakumbuka daima maelfu ya wahanga wa mauwaji ya Beni, mwenyekiti wa mashirika ya kiraia katika mji wa Beni, mwanasheria Pepin Kavota, ametoa wito kwa viongozi wa serikali kuu na pia za majimboni, kuchunguza na kuelezea pesa zilizochangishwa na makundi mbalimbali ya wakaazi, ili kujenga eneo la ukumbusho katika mji huu:

Mbali na shughuli ya leo ya kusafisha makaburi, viongozi wa mashirika ya kiraia katika mji na wilaya ya Beni, wameandaa shughuli nyengine mbalimbali katika maeneo yote yanayoshuhudia mauwaji ili kuwakumbuka waliopoteza maisha yao.

Tangu kuanza kwa mauwaji ya kukatwa kwa mapanga katika eneo hili, zaidi ya watu elfu nne wameshapoteza maisha, huku nyumba, pikipiki pamoja na magari yakichomwa moto na waasi wa ADF.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW