1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUhispania

Mapadri wa Uhispania waliwadhulumu kingono watoto 200,000

28 Oktoba 2023

Ripoti iliyochapishwa Ijumaa hii imesema karibu Wahispania 200,000 wamekiri kudhulumiwa kingono na padri wa Kanisa Katoliki walipokuwa wadogo.

Hatua za uchunguzi wa visa vya matukio ya udhalimu wa kingono unaofanywa na viongozi wa dini umesaidia kuponya majeraha na hatua kuchukuliwa
Hatua za uchunguzi wa visa vya matukio ya udhalimu wa kingono unaofanywa na viongozi wa dini umesaidia kuponya majeraha na hatua kuchukuliwaPicha: Susana Vera/REUTERS

Watu 8,000 walihojiwa na tume ya haki za binaadamu iiyoundwa nchini Uhispania kuchunguza visa hivyo na kugundua kwamba karibu asilimia 0.6 ya watu wazima kwenye taifa hilo la watu milioni 39 walidhulumiwa kingono na padri.

Kaimu Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez amesema kutolewa kwa ripoti hiyo ni "hatua muhimu" katika historia ya kidemokrasia ya nchi hiyo.

Ripoti hiyo yenye kurasa 777, unajumuisha pia matamshi ya wahanga 487 waliosema wanakabiliwa na changamoto za kihisia zilizosababishwa na mikasa hiyo.

Ripoti hiyo aidha imetoa wito kwa serikali kuandaa fungu la kuwasaidia wahanga, ambao asilimia 65 miongoni mwao wakiaminika kuwa ni wanaume.