1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kumeripotiwa mlipuko nje ya uwanja wa ndege wa Kabul

Sylvia Mwehozi
26 Agosti 2021

Kumetokea mlipuko nje ya uwanja wa ndege wa Kabul, ambako maelfu ya watu wamekusanyika kujaribu kuikimbia nchi kwa kutumia ndege za mataifa ya Magharibi tangu Taliban wadhibiti nchi mapema mwezi huu.

Afghanistan I Explosion am Flughafen in Kabul
Picha: Wali Sabawoon/AP/picture alliance

Msemaji  wa wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon, John Kirby amethibitisha taarifa za mlipuko huo nje ya uwanja wa ndege wa Kabul lakini akasema madhara ya mlipuko huo bado hayajafahamika.

Mataifa ya magharibi yalikuwa tayari yameonya juu ya uwezekano wa shambulio katika uwanja wa ndege wa Kabul katikati mwa juhudi za uhamishaji mkubwa wa watu. Nchi kadhaa ziliwatolea mwito raia wake kuepuka maeneo ya uwanja wa ndege, ambako maafisa walidai kulikuwa na kitisho cha bomu la kujitoa muhanga.Taliban waonya kuongezwa muda wa vikosi vya kigeni

Tahadhari hiyo iliyotolewa siku ya Jumatano inalihusisha kundi la Afghanistan lenye mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS ambalo kuna uwezekano kuimarika kwake kumetokana na kuachiwa kwa wafungwa wengi wa Taliban na uvamizi wao kote nchini.

Kaimu balozi wa Marekani nchini Afghanistan Ross Wilson naye alinukuliwa akisema kuwa taarifa za kuwepo na kitisho cha usalama zilikuwa za kuaminika na za haraka, alipozungumza na kituo cha utangazaji cha ABS kutokea mjini Kabul.

Umati bado umejazana uwanja wa ndege wa KabulPicha: Wali Sabawoon/AP Photo/picture alliance

Alipoulizwa juu ya ripoti za kwamba zoezi hilo linaweza kukamilika kesho Ijumaa, Wilson alikataa kusema mengi lakini akadoekza kuwa "zipo njia nyingine salama za kufika uwanja wa ndege kwa Wamarekani ambao bado wanataka kuondoka". Kaimu huyo aliongeza kuwa "bila shaka kutakuwa na hatari kwa Waafghani ambao watashindwa kuondoka baada ya muda wa mwisho wa Biden".

Waziri wa mambo ya nje Antony Blinken alikadiria kwamba karibu Wamarekani 1,500 bado wanasubiri kuhamishwa katikakati mwa ongezeko la tahadhari za kitisho cha ugaidi katika uwanja wa ndege.Takriban raia 400 wa Afghanistan waliohamishwa wafikishwa Korea Kusini

"Ni vigumu kuelezea ugumu na hatari ya juhudi hizi. Tunafanya kazi katika mazingira hatarishi katika mji na nchi ambayo sasa inadhibitiwa na Taliban na uwezekano wa shambulio la IS. Tunachukua kila tahadhari lakini kuna kitisho kikubwa".

Canada imesema imetangaza kumaliza operesheni za kuwahamisha watu kutoka nchini Afghanistan. Urusi nayo imewahamisha takribani watu 360 huku kiasi cha raia wake 1,000 wakiamua kusalia nchini humo kulingana na taarifa za shirika la habari la TASS.

Taarifa za shirika la habari la Ujerumani dpa, zinasema zoezi la kuwahamisha raia wa Ujerumani karibu linafikia ukingoni na linaweza kukamilika kesho Ijumaa.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW