1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kumi wauwawa katika shambulio Ethiopia

14 Septemba 2022

Maafisa nchini Ethiopia wanasema watu 10 wameuwawa baada ya shambulizi la pili la angani kutokea katika mji huo wa kaskazani mapema leo, shambulio hilo limetajwa pia kujeruhi watu kadhaa

 Äthiopien Luftangriff  in Mekele, Tigray
Picha: Million Haileselassie/DW

Maafisa nchini Ethiopia wanasema watu 10 wameuwawa baada ya shambulizi la pili la angani kutokea katika mji huo wa kaskazani mapema leo.

Dokta Fasika Amdeslasie amesema miili ya waliouwawa imepelekwa hospitali ya Makelle na majeruhi 10 hospatali nyingine ya Ayder.

Shambulizi hilo linaelezwa kuwa ni kama la ndege inayorushwabila ya rubani. Msemaji wa jeshi la Ethiopia Kanali, Getnet Adane na Msemaji wa serikali Legesse Tulu hawakuweza kupatikana mara moja kuelezea shambulizi hilo.

Mnamo siku ya Jumapili, Chama cha Ukombozi cha Watu wa Tigray TPLF kilisema kipo tayari kwa usitishaji mapigano na itakubali mchakato wa amani unaoongozwa na Umoja wa Afrika, kuondoa kikwazo katika mazungumzo na serikali ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.

Soma zaidi:TPLF yasema iko tayari kwa mazungumzo ya amani Ethiopia

Serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed bado haijajatoa kauli rasmi juu ya hali inayoendelea huko Tigray, huku jumuiya ya kimataifa ikishinikiza pande zinazozozana kuchukua fursa hiyo kwa ajili ya amani.

Afisa mkuu wa hospitali ya rufaa ya Ayder huko Makele Kibrom Gebreselassie,ameliambia shirika la habari la AFP katika ujumbe mfupi wa simu kwamba watu 14 walijeruhiwa

Ethiopia yatangaza hali ya hatari

01:20

This browser does not support the video element.

"Idadi ya waliofariki imeongezeka hadi 10." Alisema Gebreselassie na kuongeza kwamba shambulio la kwamba lilijeruhi wanawake wawili na baadae kufuatiwa na shambulio la pili.

Mamlaka ya Tigray imesema shambulio hilo ikiwemo na lingine la ndege zisizo na rubani siku ya JumanneChuo Kikuu cha Mekelle lilisababisha majeruahi na uharibifu mkubwa wa mali.