1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuna haja kubwa ya kuhakikishwa haki sawa kati ya wanawake na wanaume katika Ujerumani

Manasseh Rukungu3 Novemba 2004

Tarakimu za wataalamu zinasema wanawake katiika Ujerumani huwapita wanaume wakati huu katika maswala ya elimu, kila mwanamke wa pili huchukua masomo katika chuo kuikuu baada ya kumaliza shule. Tatizo lao kubwa kabisa la pamoja ni namna ya kuoanisha shuguli za familia na ajira.

Wanawake hupata mishahara midogo sana kuliko wanaume wakati wakifanya kazi ya aina sawa.
Wanawake hupata mishahara midogo sana kuliko wanaume wakati wakifanya kazi ya aina sawa.Picha: Bilderbox

Kulingana na utafiti wa wataalamu kiasi ya asilimia 40 ya wanawake katika Ujerumani, haitaki tena kusikia juu ya uzazi. Kwa sababu hii katika mwaka uliopita wa 2003, Ujerumani ilikuwa na idadi dogo kabisa ya watoto waliozaliwa hasa ikukumbukwa kwamba, kwa wastani mwanamke mmoja alijifungua mtoto mmoja au wawili tu. Kwa sababu hii wataalamu wanaiangalia hali hii kama ni kitendawili, na wanasiasa wanajaribu kuwabebeleza wanawake kukubali uzazi kwa msaada wa kifedha. Lakini tatizo kubwa hasa linalowaumiza vichwa wanawake, ni uhaba mkubwa wa nafasi za kuwalea watoto katika shule za kindergarten. Baadhi ya wanawake husema, ama watoto au kazi.

Bibi Tullia mwenye umri wa miaka 18, kwa mfano, yuko karibu kumaliza darasa la 12 na ana mipango tele kichwani mwake kama vile kujiendeleza kielimu katika chuo kikuu na kuhitimu kazi ya kimataifa. Hadi sasa hakuwahi kuingiwa akilini na haja ya kupata watoto wala kuwa na familia, kama anavyosimulia:

Hali bora kabisa ingekuwa ni washirika wote wawili, mume na mke, kuwa na kazi, hata ikiwa ni ya mchana kutwa, na hata ikiwa tungewajibika kujinyima baadhi ya shuguli za kimaisha. Kwa maneno mengine mume na mke wanabidi kuwa na hali ya kuendesha maisha ya kuwaridhisha kwa namna sawa. Mwisho wa kumnukuklu Bi.Tullia.

Kinachowakaa nyoyoni hasa wanawake wengi vijana; ni kujihakikishia kwanza msingi wa kumpatia msaada wa pesa na kujiendeleza kikazi, ijapokuwa baadhi yao pia huingiwa na fikra ya kuunda familia. Lakini tatizo lao kubwa, ni kutokujua ni nani atakayebakia nyumbani kama mlezi, baba au mama? Ni nani atakayekuwa tayari kuacha kazi yake kwa ajili ya familia? Wanaume wengi wa Ujerumani wanashindwa kubakia nyumbani kama walezi, kwa sababu shabaha zao muhimu huwa zama hizi ni kutembea ulimwenguni na kutengeneza pesa. Au Philipp ana maoni mengine? Anasema:

Shabaha niliyo nayo ni kwamba, ni kupata nafasi za kutekeleza masilahi yangu, kama vile kuwa na nyumba ya binafsi, kuwa na familia au ghari la kunitembeza. Pia ningependa kuwa na mke, ambaye angekuwa akiwachunga watoto wangu wakati nikiwa nje. Mwissho wsa kumnukulu Bw.Philipp.

Huu ni ukweli wa kusikitisha, kwani, ijapokuwa kuna mashindano ya kuwania nafasi za haki sawa, macho ya wanaume wengi huwa ni kupata mwanamke ambaye yuko tayari kujinyima mengi kwa ajili yake, yawe yanahusu mambo ya msaada wa gharama za maisha, kujiendeleza kikazi au uhuru wa binafsi. Lakini nani atakuwa akiwashugulikia watoto? Bibi Tullia tuliyemsikiliza hapo kitambo, anasema:

Hii kwa kweli ni hali gumu, na katika upande mmoja ninaweza kuielewa, kwa sababu kila mmoja, mume na mke, anazingatia katika safu za mbele masilahi yake ya binafsi. Mwanamke aliyehitimu elimu ya juu na ana kazi inayomridhisha, huhisi kutendewa isivyohaki, wakati anapowajibika kubakia nyumbani kama mlezi wa watoto pekee. Ndio maana unakuta baadhi ya wanawake wanaofanya kazi nusu siku, ambayo hwabebesha mzigo wa kazi za aina mbili, zile za nyumbani na za ofisini au kiwandani. Kwa mujibu wa tarakimu za utafiti, ni asilimia 3 na nusu tu ya wanawake katika Ujerumani inayofanya kazi muhimu kama zile za uongozi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW