1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Al Shabaab yashambulia na kuua askari 8 Kenya

14 Juni 2023

Askari wanane wa jeshi la polisi la Kenya wameuwawa katika shambulio lililofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi la itikadi kali la Alshaabab,siku ya Jumanne.

Somalia Militants Twitter
Picha: picture alliance / AP Photo

Tukio hilo lilitokea jana katika kaunti ya Garissa mashariki mwa Kenya, eneo ambalo linapakana na Somalia ambako kundi hilo la Alshabab limekuwa likiendesha hujuma za umwagaji damu dhidi ya serikali dhaifu ya mjini Mogadishu ,kwa zaidi ya miaka 15.

Kwa mara ya kwanza Kenya ilipeleka wanajeshi wake nchini Somalia mwaka 2011 kukabiliana na wanamgambo hao, wanaofungamana na mtandao wa kimataifa wa kigaidi wa Alqaeda.

Soma pia:Al-Shaabab yatishia kuishambulia Kenya

Kwa sasa nchi hiyo ni mchangiaji mkubwa wa wanajeshi katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika, kinachopambana na kundi hilo.

Hata hivyo, Kenya imejikuta ikikabiliwa na msururu wa hujuma za mashambulio ya ulipizaji kisasi ikiwemo, tukio la mwaka 2013 la kutekwa kwa jengo la maduka ya Supermaket la Westgate jijini Nairobi,ambako watuu 67 waliuwawa.

Lakini pia kuvamiwa na kutekwa kwa chuo kikuu cha Garissa mnamo mwaka 2015 ambako watu 148 waliuwawa.

 Hujuma za Al-shabab dhidi Somalia

Ndani ya Somalia kundi hilo la AlShabaab limeendelea kufanya mashambulio ya umwagaji damu licha ya kuwepo operesheni kubwa iliyoanzishwa mwaka jana.

Kwanini Al-Shabab inawatia hofu wasomali?

01:30

This browser does not support the video element.

Mwezi Agosti vikosi vya serikali vikiungwa mkono na wanajeshiwa Umoja wa Afrika,wa ujumbe unaojulikana kama ATMIS, viliendesha oparesheni dhidi ya kundi hilo.

Katika moja ya mashambulio mabaya zaidi ya hivi karibuni dhidi ya ujumbe huo,ni yale yaliyowalenga wanajeshi wa kikosi cha Uganda na 54 kuuwawa.

Soma pia:Uganda yathibitisha kupoteza wanajeshi shambulio Somalia

Wanamgambo hao wa Al-Shabaab,waliovamia kambi ya Umoja wa Afrika Mei 26,nchini Somalia.

Na mnamo siku ya Jumamosi mwishoni mwa wiki iliyopita polisi ya Somalia ilisema raia saba waliuwawa katika tukio la kutekwakwa muda wa saa sita katika hoteli moja iliyoko kando ya bahari mjini Mogadishu na kundi hilo la wanamgambo la Al Shabab.

   

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW