1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas yasema mazungumzo ya kusitisha vita yanaendelea

15 Julai 2024

Kundi la wanamgambo wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza la Hamas, limesema mazungumzo kuhusu usitishaji mapigano yanaendelea na Kamanda wake wa kijeshi Mohammed Deif yuko katika hali nzuri kiafya.

Hali ya kiutu kwenye Ukanda wa Gaza
Hali ya kiutu kwenye Ukanda wa Gaza.Picha: EYAD BABA/AFP via Getty Images

Taarifa hiyo ya Hamas ilitolewa jana, siku moja baada ya jeshi la Israel kufanya mashambulizi yaliyomlenga kamanda huyo wa Hamas ambayo imeleezwa na maafisa wa afya kwamba yaliwauwa takriban watu 90 wakiwemo watoto.

Mnamo siku ya Jumamosi waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema bado hawana uhakika ikiwa Deif ameuwawa. Mohammed Deif anatajwa kuwa ndiye kinara aliyepanga shambulio la Oktoba 7 dhidi ya Israel lililosababisha vita vya Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW