1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

IS yakiri kuhusika na shambulizi la bomu nchini Pakistan

1 Agosti 2023

Tawi la kundi la Dola la Kiislamu la nchini Afghanistan limedai kuhusika na shambulizi la bomu la kujitoa mhanga nchini Pakistan ambalo liliwauwa watu 54.

Jamaa na waombolezaji wanabeba jeneza la mwathiriwa aliyeuawa katika shambulizi la Jumapili la mlipuaji wa kujitoa mhanga katika wilaya ya Bajur Khyber Pakhtunkhwa, Pakistan, Jumatatu, Julai 31, 2023.
Mazishi ya wahasiriwa wa shambulio kubwa la bomu la kujitoa mhanga nchini Pakistan ambalo lililenga mkutano wa mhubiri anayeunga mkono kundi la Taliban Picha: Mohammad Sajjad/AP/picture alliance

Shambulizi hilo lilitokea katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi wa chama kinachounga mkono kundi la Taliban. Lilikuwa moja ya mashambulizhi makubwa kabisa kulikumba eneo hilo katika miaka ya karibuni. Kundi la IS la Mkoa wa Khorasan limetoa taarifa hiyo jana likisema mlipuaji wake alijilipua Jumapili katika hafla hiyo ya mji wa kaskazini magharibi wa Bajur.

Shambulizi hilo ni sehemu ya vita dhidi ya demokrasia inayokiuka uislamu

Lilisema shambulizi hilo ni sehemu ya vita vinavyoendelea vya kundi hilo dhidi ya aina ya demokrasia linazoziona kuwa zinakwenda kinyume na Uislamu. Mapema jana Mamia ya waombolezaji nchini Pakistan walishiriki mazishi ya wahanga wa shambulizi hilo

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW